Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11 Januari, 2019 ameongoza mapokezi ya ndege mpya aina ya Airbus A220-300 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha huduma za usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Ndege hiyo ni ya pili ya aina ya Airbus 220-300 kununuliwa na Serikali kwa ajili ya ATCL na ni ndege ya 6 kuwasili hapa nchini kati ya ndege 7 ambazo Serikali ya Awamu ya Tano imezinunua kwa lengo la kuimarisha usafiri wa anga, kukuza utalii, kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi.

Sherehe za mapokezi ya ndege hiyo zimefanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal One) Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Pamela O’donnel, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wabunge, viongozi wa Dini, viongozi wa siasa, wafanyabiashara, viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda.

Akizungumza baada ya kuipokea na kuizindua ndege hiyo, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Watanzania wote kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake ikiwemo kununua ndege 7 zilizowezesha kuimarishwa kwa ATCL pamoja kutekelezwa kwa miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) na mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji, na kwamba kwa mwendo huu mambo mengine mengi makubwa yanakuja.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi na wafanyakazi wote wa ATCL kwa kazi nzuri wanayofanya wakiwemo Marubani vijana wa Kitanzania watatu walioendesha ndege hiyo kutoka Montreal nchini Canada hadi Jijini Dar es Salaam Tanzania, na amebainisha kuwa hayo ni matunda ya kununua ndege mpya na kuimarisha ATCL.

“Tumeambiwa hapa tangu tuanze kununua ndege hizi ATCL imeongeza idadi ya Marubani kutoka 11 hadi 50, walioajiriwa ni vijana wetu wa Kitanzania, na kwa ujumla wafanyakazi wapya wa ATCL walioajiriwa ni 380, hivi kama tusingenunua ndege hizi vijana hawa wangeendesha nini? Wangeendesha matoroli? Lakini sasa wamepata ajira wananufaika wao na familia zao au jamaa zao” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa ndege hizi zote zimenunuliwa kwa fedha za Watanzania kwa asilimia 100, na amewataka Watanzania wote kuelewa kuwa maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na kwamba hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea kwa kutegemea misaada.

“Tunahitaji misaada lakini iwe ni misaada ya kutuwezesha kusonga mbele kimaendeleo na kujitegemea na sio kutulemaza, sekta binafsi pia tunaihitaji lakini iwe ni sekta binafsi ya manufaa kwa Taifa

  • ATCLimekuwa Shirika la kwanza la barani Afrika  kununua Ndege aina ya Airbus A200-300ATCLimekuwa Shirika la kwanza la barani Afrika kununua Ndege aina ya Airbus A200-300
  • Kiashiria cha ndege Mpya ikiwasiliKiashiria cha ndege Mpya ikiwasili