Tarehe 02 Aprili 2024, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Msumbiji alitembelewa na Mhe. Ndamage Donat, Balozi wa Jamhuri ya Rwanda - Msumbiji.
Mhe. Balozi Donate alifika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Maputo kujitambulisha kufuatia kuteuliwa hivi karibuni na nchi yake kuiwakilisha nchini Msumbiji.
Katika Mkutano huo, Viongozi hao wawili walikubaliana kushirikiana kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya nchi zao mbili, ambazo pia ni miongoni mwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zenye uwakilishi nchini Msumbiji.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania -- Maputo
03 April, 2024