Mhe. CP. Hamad K. Hamad, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, ameungana na Mabalozi wengine na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Msumbiji katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa nchini humo inayofanyika tarehe 3 Februari kila Mwaka.
katika Maadhimisho hayo, Mhe. Daniel F. Chapo ndiye alikua mgeni rasmi na kuongoza washiriki wengine katika zoezi la kuweka mashada ya maua katika makaburi ya waasisi waliopigania uhuru na viongozi wa awali wa Taifa la Msumbiji akiwemo Hayati Eduardo Mondlane na Samora Machel.
