Tarehe 25-26 Februari, 2026, jijini Maputo, Msumbiji, Mheshimiwa CP. Hamadi Khamis Hamad, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ameiwakilisha Tanzania kwenye Mkutano wa Biashara wa Umoja wa Afrika ikiwa ni maandalizi ya ushiriki wa nchi za Afrika kwenye Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Biashara wa Shirika la Biashara Duniani (WTO M14).
Pamoja na masuala mengine Mkutano huo umejadili kuhusu umuhimu wa maboresho ya Shirika la Biashara Duniani, ikiwemo kuweka usawa katika biashara, maboresho ya mfumo wa utatuzi wa migogoro na pendekezo la Umoja wa Afrika kupata nafasi ya kudumu kwenye Shirika hilo.
Vilevile, Mkutano huo umezungumzia changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea (LDCs) hususan Nchi za Afrika kwenye Multilateral Trading System, ikiwemo digital gap kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Hivyo nchi hizo zimeahidi kuweka mifumo ya Afrika kuwa active player kwenye e-commerce duniani.


