Tarehe 31 Machi 2026, Mhe. CP. Hamad K. Hamad, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, alikutana na Mhe. Nicolas Randin, Balozi wa Uswizi, katika Ofisi ya Ubalozi jijini Maputo.
Kikao hiki kililenga kufahamiana rasmi na kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Uswizi, ikizingatiwa Balozi Randin aliteuliwa kuhudumu nchini Msumbiji mnamo Septemba 2025.
Mhe. Balozi CP. Hamad alimkaribisha Balozi wa Uswizi rasmi na kumpongeza na akasisitiza umuhimu wa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo na fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania.
Kwa upande wake, Balozi Randin alimshukuru Mhe. Balozi kwa mapokezi mazuri na kueleza vipaumbele vya Uswizi vya kuchangia maendeleo ya nchi malimbali za Afrika, hususan ukanda wa kusini mwa Afrika.
Viongozi hao pia waligusia mchango wa Msumbiji kama nchi mwenyeji katika kukuza maendeleo ya kikanda na ushirikiano wake na Tanzania. Mazungumzo haya yameweka msingi wa ushirikiano madhubuti na wa muda mrefu kati ya Tanzania na Uswizi.