Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, amekutana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane Cha Msumbiji ulioongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Doutor Manuel Guilherme Junior, leo tarehe 13 Februari, 2024.
Katika mazungumzo yao, pande mbili zilikubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano (kati ya Tanzania na Msumbiji) katika sekta ya Elimu, hususan kuanzishwa Darasa la Kiswahili Chuoni hapo na Darasa la Kireno katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam..