anzania imeshiriki Maonesho ya 61 ya Biashara yaKimataifa ya Maputo (FACIM 2026), yanayofanyika katikaeneo la Ricatla, Maputo, Msumbiji, katika kipindi ambachoTanzania na Msumbiji zinaendelea kuimarisha uhusiano wakiuchumi na kibiashara.
Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi tarehe 31 Agosti 2026 na Mhe. Daniel Francisco Chapo, Rais wa Jamhuri yaMsumbiji. Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi waMaonesho hayo, Mhe. Chapo amesisitiza kuwa FACIM nijukwaa muhimu la kukuza uchumi na kuimarisha ushirikianowa kibiashara kati ya Msumbiji na mataifa mengine.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya Msumbiji inaendeleakufanya maboresho katika sera na mifumo mbalimbali yauwekezaji kwa lengo la kuvutia wawekezaji zaidi na kuwekamazingira rafiki kwa biashara na uwekezaji.
Ushiriki wa Tanzania katika FACIM 2026 unaratibiwa naUbalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchiniMsumbiji kwa kushirikiana na Tanzania Trade Development Authority (TANTRADE). Katika maonesho hayo, Tanzania inashiriki ikiwa na takribani kampuni na taasisi nane (8) kutoka sekta za umma, sekta binafsi pamoja na wajasiriamaliwadogo na wa kati, ikiwemo TRA, Bodi ya Chai Tanzania, Farmers Center, Farmbase Ltd., SWAENERGY, Cutoff Recycle na The Line Group ambao wanaonesha bidhaa, huduma na fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji kutokaTanzania.
Lengo kuu la Tanzania kushiriki kwenye Maonesho yaFACIM 2026 ni kukuza biashara na uwekezaji kati yaTanzania na Msumbiji, pamoja na kuwaunganishawafanyabiashara, wawekezaji na wadau wa sekta mbalimbalikutoka nchi hizi mbili ili kutengeneza fursa mpya za ushirikiano wa kibiashara.
Katika Maonesho hayo, Tanzania inatangaza huduma nabidhaa zenye chapa ya “Made in Tanzania” kama chapainayowakilisha bidhaa zinazozalishwa nchini, ubunifu nauwezo wa Tanzania katika kuongeza thamani ya mazao namalighafi.
Washiriki kutoka Tanzania wanaonesha fursa katika maeneombalimbali, ikiwemo kilimo na uongezaji thamani, chai, nishati, teknolojia na mabadiliko ya kidijitali, urejelezaji, bidhaa za viwandani, nguo na bidhaa za utamaduni (culture), pamoja na huduma mbalimbali zinazoweza kuunganishawafanyabiashara wa Tanzania na Msumbiji.
Ushiriki wa Tanzania unaongozwa na kaulimbiu ya“Mapinduzi ya Kidijitali na Nishati kuelekea Uchumi Endelevu”, inayolenga kuonesha nafasi ya teknolojia, nishatina ubunifu katika kukuza uchumi endelevu na kuongezaushindani wa bidhaa na huduma za Tanzania katika masokoya kikanda na kimataifa.
Tanzania inaendelea kutambua Msumbiji kama jirani namshirika muhimu wa kiuchumi, na inatumia FACIM 2026 kama jukwaa la kuongeza mwonekano wa bidhaa za Tanzania, kutangaza fursa za uwekezaji na kufungua milangoya ushirikiano mpya kati ya wafanyabiashara wa Tanzania naMsumbiji.

_1000_666shar-50brig-20.jpg)

_1000_750shar-50brig-20.jpg)
_1000_750shar-50brig-20.jpg)
