Mbabane, 28 Septemba 2026 — Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Eswatini, Mhe. CP. Hamad Khamis Hamad, amefanya Ziara ya Heshima kwa Waziri Mkuu wa Ufalme wa Eswatini, Mhe. Russell Dlamini.
Mazungumzo ya viongozi hao yalilenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Eswatini, hususan katika biashara na uwekezaji, utalii, elimu, kilimo, miundombinu, Kiswahili na ushirikiano wa kikanda kupitia SADC.
Waziri Mkuu alieleza fursa zilizopo kwa kampuni za Tanzania kushiriki katika miradi ya maendeleo nchini Eswatini, pamoja na umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa utalii na kuanzisha vifurushi vya pamoja vya utalii kati ya nchi hizi mbili.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa Kiswahili kama nyenzo ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano barani Afrika.
Mazungumzo hayo pia yalihusu mwaliko wa Mheshimiwa Mfalme Mswati III kutembelea Tanzania, ikiwemo fursa ya kushuhudia uhamiaji mkubwa wa wanyamapori katika Serengeti.
Tanzania na Eswatini: Kuimarisha Urafiki, Kupanua Ushirikiano, Kujenga Fursa.
#TanzaniaEswatini #Diplomasia #Ushirikiano #DiplomasiaYaUchumi #Utalii #Kiswahili #SADC